MABINGWA mara nne wa kombe la Mataifa ya Afrika,
timu ya taifa ya Ghana imepoteza mechi yake ya kwanza ya kundi C ya michuano ya
Mataifa ya Afrika inayoendelea Guinea ya Ikweta kwa kufungwa bao 2-1 na
Senegal.
Dakika za mapema (dk 14’) Andre Ayew aliifungia
bao la kuongoza Ghana kabla ya Simba Wateranga kusawazisha katika dakika ya
Mame Biram Diouf katika dakika ya 58’.
Moussa Sow aliwanyanyua mashabiki wa Senegal
katika dakika ya 90’ akiandika bao la kuongoza.
Mechi ya pili ya kundi C imemalizika usiku huu kwa
Algeria kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Afrika kusini.
Huu ni ushindi wa kwanza mkubwa katika mechi sita zilizocheza.
Afrika kusini walikuwa wa kwanza kuandika bao la
kuongoza katika dakika ya 51’ kupitia kwa Thuso Phala, lakini Algeria walifuta
bao hilo dakika ya 68’ kutokana na Thulani Hlatshwayo kujifunga.
Dakika ya 72’ Faouzi Ghoulam aliiandika bao la
pili Algeria na baadaye Islam Slimani alihitimisha sherehe ya ushindi.
Gabon walipata matokeo ya bao 2-0 dhidi ya Burkina
Faso. Timu ya pili kupata ushindi mwingine imekuwa Senegal ambayo imeshinda
2-1.
Guinea ya Ikweta wao walitoka sare ya 1-1 katika
mechi ya kundi A, wakati kundi B timu zote zilitoka sare.
Zambia walitoka sare ya 1-1 na DR Congo baadaye
Tunisi walitoka 1-1 na Cape Verde.
MATOKEO YA MECHI ZA KUNDI C
Africa Cup of Nations - Group CJanuary 19 | |||
---|---|---|---|
FT | 1 - 2 | ||
FT | 3 - 1 |
Baada ya kundi kundi C kucheza mechi za ufunguzi, leo ni zamu ya kundi D ambapo Tembo wa Pwani ya Magharibi mwa Afrika, Ivory Coast watashuka dimbani kuchuana na Guinea majira ya saa 1:00 usiku.
Mechi ya pili itapigwa majira ya saa 4:00 usiku ambapo Mali wataivaa Cameroon.
RATIBA YA LEO AFCON KUNDI D
Africa Cup of Nations - Group DJanuary 20 | |||
---|---|---|---|
19:00 | ? - ? | ||
22:00 | ? - ? |
0 comments:
Post a Comment