Saturday, January 10, 2015

Ivo Mapunda akifanya mazoezi jana uwanja wa Amaan

GOLIKIPA mkongwe wa Simba SC, Ivo Philip Mapunda amerejea kambani kufuatia kutokuwepo kwa siku tisa akikamilisha 40 za mama yake mzazi aliyefariki dunia mwishoni mwa mwezi novemba.
Mapunda alitua jana mjini Zanzibar na kuungana na wenzake katika mazoezi ya jioni yaliyofanyika uwanja wa Amaan kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi itakayopigwa usiku wa leo baina ya Simba na Polisi Zanzibar.

Akizungumza na mtandao huu, kipa huyo wa zamani wa Tanzania Prisons, Yanga, Gor Mahia ya Kenya na Saint George ya Ethiopia alisema kwasasa hayuko fiti kucheza mechi.

“Nimeingia leo (jana) hapa hapa Zanzibar na kuanza mazoezi jioni hii. Sikuwepo kwa muda siku tisa. Niliondoka tarehe moja”. Alisema Ivo. “Hapa mpaka niamshe amshe viungo, si unajua vililala kwa muda”.

Ivo ndiye aliyesimama langoni Simba ikichapwa bao 1-0 na Kagera Sugar, desemba 26 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kuamsha hasira za mashabiki wa Simba.

Goli hilo lilifungwa na Atupele Green katika dakika ya 21 akimalizia mpira wa kurushwa ambapo Mapunda alishindwa kuucheza.


Kipigo hicho kilimfukuzisha kazi kocha Patrick Phiri na mikoba yake kuchukuliwa na Mserbia, Goran Kopunovic.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video