Thursday, January 15, 2015

Manyika Peter akijifua na timu yake ya Simba katika Uwanja wa Amani Zanzibar walipokuwa wakishiriki michuano ya KOmbe la Mapinduzi.
Manyika Peter akijifua na timu yake ya Simba katika Uwanja wa Amaan Zanzibar walipokuwa wakishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.


Goli kipa namba mbili wa klabu ya Simba Manyika Peter, leo amechagulia na Kocha mkuu wa timu ya Taifa Mart Nooij kujiunga na Timu ya Taifa ya Maboresho ambayo inakabiliwa na mchezo wa kirafiki na Rwanda hapo January 22 mwaka huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza.

Mbali na Manyika pia Kiungo chipukizi wa Yanga Salum Telela amejumuishwa katika kikosi hicho kwa mara ya kwanza baada ya kuonyesha kiwango cha juu akiwa na Klabu yake hiyo ya Jangwani.

Nooij amesema kuwa Stars wataingia kambini januari 18, ambapo wachezaji 16 watakuwa kambi ya Dar es salaam na wengine 10 wataingia kambi ya Mwanza, itakapo fika januari 19, Wachezaji wote wa Dar es salaam na Mwanza wataungana kambini sehemu moja jijini Mwanza tayari kwa mechi januari 22 ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba.

Wachezaji wengine ni Aishi Manula kutoka Azam FC, Benedict Tinoco wa Kagera Sugar na Manyika Peter wote ni makipa.

Mabeki ni Miraji Adam wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicent wa Mtibwa Sugar, Gadiel Michael Mbaga wa Azam FC, Emanuel Semwanda wa African Lion, Joram Mgeveke wa Mwadui, Edward Cherles wa Yanga, Mohamed Hussein wa Simba na Salum Mbonde wa Mtibwa Sugar.

Viungo ni Salum Telela wa Yanga, Adam Paulo Salamba wa Bulyankulu SC, Hassan Banda wa Simba, Said Juma Makapu wa Yanga, Said Hamis Ndemla wa Simba, Hassan Dilunga wa Yanga, Hussein Moshi Malombe wa Geita Gold SC, Shiza Ramadhani wa Mtibwa Sugar, Omary Nyenje wa Ndanda FC, pamoja na Alfred Juma Masumbakenda wa Bulyankuru 



Source: hivisasa.co.tz

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video