Wakala wa mchezaji kinda wa Manchester United Adnan
Januzaj,De Vriese ametoboa siri kuwa Manchester United
chini ya kocha Louis Van Gaal imekaa ombi kutoka kwa miamba ya soka nchini
ufaransa Paris Saint Germain kumsajili mchezaji huyo katika dirisha dogo la
usajili.
Januzaj mwenye umri wa miaka kumi na tisa, amekuwa akiangaika kupata namba katika kikosi cha kwanza cha kocha Louis Van Gaal lakini ameishia kucheza mechi kumi na tatu pekee katika mashiandano yote msimu huu.
"Ndio,PSG wameonyesha nia ya kumsajili Januzaj kipindi hiki," wakala De Vriese aliliambia Gazeti la Foot Mercato.
Januzaj anamkataba wa kuitumikia Manchester United mpaka mwezi June 2018.
0 comments:
Post a Comment