Mama mzazi wa mtoto wa Cristiano Ronaldo amefahamika kuwa ni mwanafunzi wa Uingereza....ambaye sasa anamtaka mtoto wake.
Mpaka sasa Ronaldo ameficha siri ya jina, umri na hata Utaifa wa mzazi mwenzake kufuatia kupata haki ya kumiliki mtoto kwa malipo ya paundi milioni 10.
Hata hivyo, Gazeti la Sunday Mirror limeweka wazi kuwa mwanamke huyo ana umri wa miaka 20 ambaye anajutia maamuzi yake na amekuwa akimpigia simu mara nyingi nyota huyo wa zamani wa Manchester United akiomba nafasi ya kuonana na mtoto wake.
Mwanamke huyo aliyepata ujauzito kwa kulala na Ronaldo usiku mmoja anadai yuko tayari hata kulipa mamilioni aliyopewa, akisisitiza amebadili akili yako.
Maamuzi yake ya kumpa mtoto Ronaldo, mchezaji ghali katika historia ya mpira yamemuacha awe na msongo wa mawazo, marafiki zake wanasema, hali hiyo imesababisha ashuke kiwango kitaaluma.
Kipengele cha mkataba alichosaini na mwanasheria wa Ronaldo kinamaanisha haruhusiwi kumuambia mtu yeyote kuwa yeye ndiye mama mzazi wa mtoto wake ikiwemo na familia yake.
Alipotea baada ya kupata mimba na baada ya kuzaa aliwaambia watu alipata matatizo kidogo ya kuvimba tumbo.
Alipoomba kumona mwanaye, Ronaldo alisema anafirikiria ombi lake kama atarudisha baadhi ya pesa alizopewa.
Chanzo cha karibu cha mwanamke huyo kilisema: "Mara nyingi usiku anampigia Ronaldo. Anamlilia sana na kumbembeleza. Ronaldo hakuwa hata na mawasiliano naye, lakini kwasasa wanaongea kwenye twita"
"Anampigia hata baada ya mechi akimpongeza kwa jinsi alivyocheza, akiamini kwamba siku moja atakata rufaa, lakini Ronaldo anamtia moyo kuhusu kumuona Cristiano Jr.
"Mwanamke huyu anahisi kama ameuza roho yake. Ana maisha ya kimilionea, lakini kamwe hawezi hata kumwabia rafiki yake na familia ukweli kuhusu kilichotokea---hakika kitendo hiki kinamfanya awe mpweke".
Rafiki wa Ronaldo ambaye ana miaka 29 sasa alisema "Kwa vile hilo lilikuwa juu yake, lilikuwa chaguo lake, maamuzi yake. Alisema, "Hana haki yoyote juu ya mtoto wangu. Hatamwona tena mwanangu"
"Lakini Ronaldo anapokea simu zake, ana wasiwasi kuwa anaweza kupambana kupata haki ya kumuona mwanaye na anataka kusikia anawaza nini"
"Kwa mkataba uliosainiwa unamkaba kabisa. Lakini ana nguvu kama mama ya kupata haki ya kumuona mwanaye--kwahiyo kitu chochote kinaweza kutokea".
Marafiki wa Ronaldo wanasema, nyota huyo wa Real Madrid alikutana na mwanamke huyo katika klabu ya usiku mjini London na walifanya mapenzi katika hoteli.
Alipokuwa na mimba aliwasiliana na Ronaldo kupitia wakala wake Jorge Mendes na mambo mengine yalipigwa chini.
Mama yake Ronaldo mwenye miaka 58 Doleres na dada zake Elma na Liliana Catia walikubali kumlea mtoto huyo.
Baada ya mtoto kuzaliwa, mwanasheria wa Ronaldo alifanya mpango wa vipimo vya DNA kuthibitisha kama kweli mtoto ni wa nyota huyo raia wa Ureno.
Jambo hili lilifanyika majira ya kiangazi mwaka 2010 wakati nyota huyo aliyerithi jezi namba saba ya George Best, Eric Cantona na David Beckham akiwa Man Utd, anacheza fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini.
Julai 3 mwaka huo,Ronaldo aliitangazia dunia kuwa ana mtoto wa kiume, aliandika kwenye ukurasa wa facebook kuwa mama yake hataki kutambulishwa. Aliongeza: "Mwanangu atakiwa chini ya uangalizi wangu"
Vyombo vya habari vilimsakama Ronaldo vikitaka kujua jina la mama mzazi wa mtoto ikiwemo Paris Hilton na Realiy TV Star Imogen Thomas, lakini kamwe jina lake halikuwekwa wazi.
Kwa mara ya kwanza mtoto alioneshwa hadharani desemba 8, 2011 nchini Hispania katika mechi ya Real Madrid ambapo mama yake Ronaldo na ndugu zake walipiga picha wakiwa wamembeba.
0 comments:
Post a Comment