Thursday, January 15, 2015

Simba wakifanya mazoezi walipokuwa Zanzibar

KIKOSI cha Simba SC leo jioni kimefanya mazoezi Uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kujiandaa na mechi ya keshokutwa ya ligi kuu soka Tanzania katika uwanja huo dhidi ya wenyeji Ndanda fc ‘Mtwara Kuchele’.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio amesema wachezaji wote wapo salama na kocha Goran Kopunovic ana matumaini makubwa ya kuchukua pointi tatu muhimu.

“Tumefanya mazoezi leo jioni, kocha amewaona wachezaji wake na akasema wapo fiti. Ndanda lazima wana hofu, wameona mambo makubwa tuliyofanya kombe la Mapinduzi”.


Simba walifanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi 2015 kufuatia kuifunga Mtibwa Sugar penalti 4-3 katika mechi ya fainali iliyopigwa januari 13 mwaka huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video