
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Azam fc wanaingia kwa tahadhari kubwa katika mechi ya leo ya ligi kuu
itayopigwa uwanja wa CCM Kambarage Mkoani Shinyanga dhidi ya wenyeji Stand
United.
Meneja wa Azam fc, Jemedari Said Mzumari amesema
wanaingia uwanjani wakitambua wanacheza na moja ya timu 14 zinazogombea ubingwa
wa VPL.
“ Stand United ni moja ya timu nzuri ambazo
zilianza ligi kwa kusuasua, lakini zikapata kasi wakati ligi inaendelea”
Alisema Jemedari. “ Mechi nyingi tu wamepata matokeo mazuri, walipata matokeo
mazuri dhidi ya Simba uwanja wa Taifa, wamepata matokea ugenini dhidi ya
viongozi wa ligi ambao hawajafungwa Mtibwa Sugar”
“Pia Bukoba walipata matokeo mazuri, hii inaonesha
kwamba ni timu inayobadilika na kadri siku zinavyokwenda inazidi kuimarika,
isipokuwa sisi kama mabingwa watetezi wa kombe hili, tunaamini kuwa sisi ni
timu yenye mchanganyiko mzuri wa wachezaji katika ligi hii na ni timu imara,
tumepania kupata pointi tatu na si tatu tu, bali ni tisa katika michezo mitatu
kabla hatujasafiri kwenda Lubumbashi”.
“Tumejiandaa leo kupata pointi tatu, halafu
tutakwenda Mwanza kuchukua pointi tatu kabla ya kukwaana na Simba Dar es salaam”.
Amesema Jemedari.
0 comments:
Post a Comment