Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Barcelona
na timu ya taifa ya Ureno Luis Figo ametangaza
rasmi uwamuzi wake wa kugombea Urais katika shirikisho la mpira wa miguu
duniani Fifa mwaka huu lengo kubwa ni kumng’oa Rais aliyepo madarakani kwa sasa
Sepp Blatter.
Mwisho wa wagombea kutangaza kugombea nafasi hiyo ni alhamisi wiki hii, lakini Figo ameamua kutangaza mapema akiwa na wapambe watano wanaomsapoti kutoka Fifa.
Figo alisema anaupenda sana mpira wa miguu, ni wakati sahihi
sasa kufanya marekebisho katika shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa kwani
shirikisho hilo limekuwa na picha mbaya baada ya kutotekeleza mambo muhimu
katika mchezo wa soka.
"Naupenda sana mpira wa miguu nisingependa kuona
unadidimizwa na watu wasiopenda maendeleo yake, lakini pia kuirudisha picha
nzuri ya shirikisho ambayo imeharibiwa na viongozi ambao wapo madarakani kwa
sasa, ndio maana nimeamua kugombea nafasi ya Urais katika shirikisho,’’ Figo
aliliambia shirika la utangazi CNN.
"nimekuwa nikuzungumza na watu wengi sana ambao ni
muhimu katika mchezo wa soka kama vile wachezaji, makocha pamoja na marais wa
mashirikisho mbalimbali ya mpira na wote wanafikiria kama mimi kwamba lazima
kuwe na mabadiliko,”aliongeza Luis Figo
0 comments:
Post a Comment