Saturday, January 17, 2015



FT: YANGA SC 0 : 0 RUVU SHOOTINGS

Dakika za lala salama Yanga wanatafuta njia ya kufunga goli, lakini mabeki wa Shootings wamesimama imara

Dakika +4' za nyongeza 

Dakika ya 90' mpira umesimama baada ya mchezaji wa Shootings kufanyiwa madhambi

Dakika ya 89' kunatokea Sintofahamu baina ya kipa wa Yanga na mchezaji wa Shootings baada ya Yondani kumfanyia madhambi mchezaji pinzani

Dakika ya 83' Salvatory Ntebe  anaoneshwa kadi nyekundu

Dakika ya 81' Rajab Zahiri ameiokoa Yanga katika hatari baada ya mshambulizi wa Shootings, Abdulrahman Musaa kubaki yeye na kipa na mpira kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Dakika ya 80' si Yanga wala Shootings iliyoona lango la mwenzake

Dakika ya 78' Niyonzima anapiga mpira wa adhabu ndogo kutoka winga ya kulia lakini mabeki wa Shootings wanaokoa

Dakika ya 75' milango ya timu zote bado ni migumu na Yanga wanashindwa kutumia kona waliyopata baada ya mabeki wa Shootings kuokoa

Dakika ya 73' Yanga wanapata kona, lakini kipa Abdallah Rashind ameanguka chini na anatibiwa

Dakika ya 71' Hussein Javu anaingia kuchukua nafasi ya Coutinho

Dakika ya 68' Jerome Lambele anaingia kuchukua nafasi ya Mwita Kemalonge

Dakika ya 68' Mpira umesimama baada ya mchezaji wa Shootings kufanyiwa madhambi

Dakika ya 65' Msuva anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Daniel 'Danny' Davis Mrwanda

TAIFA: Dakika ya 61' hakuna timu ilipata goli kati ya Yanga na Ruvu Shootings
................................

NDANDA 0 : 2 SIMBA SC
....................kutoka Mtwara, Elius Maguri anaifungia Simba bao la pili katika dakika ya 52 akipokea pasi ya Danny Sserunkuma.
..............
Dakika ya 55' Yahya Tumbo anakwenda benchi kwa upande wa Ruvu Shootings nafasi yake inachukuliwa na Baraka Mtuwi

Dakika ya 51' bado milango ni migumu

Dakika ya 47' hakuna timu iliyoona lango baina ya Yanga na Ruvu Shootings

.........UWANJA WA TAIFA YANGA 0 : 0 RUVU SHOOTINGS

HT: STAND UNITED 0 : 1 AZAM FC

DAKIKA YA 43' Azam fc wanaandika bao la kuongoza kupitia kwa kiungo Frank Domayo 'Chumvi'

KUTOKA CCM KWAKWANI TANGA dakika ya 45 hakuna timu iliyoona lango la mwenzake baina ya Mgambo JKT na Tanzania Prisons

KUTOKA CCM Kambarage Shinyanga dakika ya 35 kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake baina ya Stand United na Azam fc

KUTOKA NAGWANDA SIJAONA MTWARA...Mpira ni mapumziko Simba wakiwa mbele kwa goli moja lililofungwa na Danny Sserunkuma katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Elius Maguri
...........................................

HT: YANGA 0 : 0 RUVU SHOOTINGS

Dakika za mwishoni kabisa za nyongeza Yanga wamepata kona mbili mfululizo, lakini hazijazaa matunda

Dakika ya mwisho ya nyongeza kumetokea piga nikupige eneo la Shootings, lakini mabeki wanaokoa.

Dakika 45' zimekamilika na mwamuzi anongeza dakika tano za nyongeza

Dakika ya 44' Shootings wamepoteza nafasi nzuri ya kufunga

Dakika ya 40' Msuva anakosa nafasi nyingine baada ya kuwekewa mpira na Edward Charles. Mpira huo ulitokana na mpira wa kona kufuatia shuti la Tambwe kuokolewa na kipa Rashid

Dakika ya 39' Msuva anakosa bao akiwa yeye na kipa

Dakika ya 36' Yanga wanapata kona ambayo haizai matunda

Dakika ya 33' Coutinho anapiga mpira wa adhabu ndogo unaowababatiza mabeki wa Shootings na kumchanganya kipa Rashid, lakini anajitahidi kuokoa

Dakika ya Dakika ya 25' Coutinho amekosa bao baada ya kichwa chake kutoka nje ya lango akiunganisha krosi ya Niyonzima kutoka winga ya kulia

Dakika ya 24' hakuna timu iliyoona lango la mwenzake

Dakika ya 19' Tambwe amefunga goli kwa mkono mwamuzi anakataa na kumuonesha kadi ya njano

Dakika ya 18' Saimon Msuva anaoneshwa kadi ya njano

Dakika ya 17 mpira umesimama baada ya Msuva kumfanyiwa madhambi mchezaji wa Shootings ambaye yuko chini

Dakika ya 12' Andrey Coutinho amepiga mpira wa adhabu ndogo ndani ya eneo la 18, lakini mlinda mlango Rashid Abdallah ameokoa

Dakika ya 6' kipindi cha kwanza Yanga wanagongeana pasi eneo lao, lakini wanashindwa kuvuka kirahisi eneo la Shootings kutokana na ulinzi waliowekewa

Dakika ya 4' Yanga wameanza kwa kasi wakifika mara kadhaa langoni kwa Shootings lakini mipango haijawa sawa

Yanga wamepata kona sekunde kadhaa lakini haijazaa matunda

Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa Yanga wakiwa wa kwanza kugusa mpira, Tambwe na Sherman

Wachezaji wanasalimiana tayari kwa kuanza kipute

Wachezaji wa timu zote wameingia uwanjani tayari kwa kukaguliwa na waamuzi

YANGA SC 0 : 0 RUVU SHOOTINGS

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video