Na Frank M Mgunga, Dar es salaam
Klabu ya maafande wa Jkt Ruvu imetamba kuibuka na ushindi
dhidi ya klabu ya wekundu wa msimbazi Simba ambayo imetoka kujeruhiwa na klabu
ya Mbeya City baada ya kufungwa magoli mawili kwa moja katika uwanja wa Taifa
jijini Dare s salaam mitanange ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Kocha msaidizi wa wapiga kwata hao Greyson Haule ameiambia MPENJA BLOG kuwa wamejipanga vizuri kuikabili Simba wikiendi hii huku wakitumia mwanya
wa majeruhi waliyoyapata kutoka kwa wagonga nyundo Mbeya City.
“Sisi tumejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya
simba wikiendi, kwani tunaelewa ni mchezo mgumu kwetu sisi lakini tutafanya
kila kinachowezekana kuhakikisha tunaibuka na ushindi katika mchezo huo na
kupata pointi tatu muhimu,”alisema Greyson Haule.
Jkt Ruvu waliweza kumsajili mchezaji Betram Mombeki kutoka
katika klabu ya wekundu wa msimbazi Simba, mchezaji ambaye mara nyingi amekuwa
akizichachafanya ngome za ulinzi za timu pinzani msimu huu na msimu uliopita
akiwa na wekundu wa msimbazi.
0 comments:
Post a Comment