Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kiungo Mrundi Pierre Kwizera amejiunga na Sofapaka FC ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL), imefahamika.
Kwizera alitemwa Simba SC dakika za mwisho za usajili wa dirisha dogo msimu huu (Desemba 14, 2014) pamoja na Mrundi mwenzake Amisi Tambwe ili kuwapisha Waganda Simon Sserunkuma na Juuko Murshid.
George Banda, meneja wa mchezaji huyo, amesema Kwizera atatua Kenya leo akitokea kwao Burundi ingawa kumeibuka utata katika upatikanaji wa Uhamisho wa Kimataifa.
Utata uliooibuka katika kupata ITC ya nyota huyo umeelezwa na Banda kuwa walipowasiliana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana mchana wameambiwa ilishatumwa klabu ya Rayon ya Rwanda.
"Mimi kama meneja wa Kwizera, ninajua hajasaini wala kuzungumza na Rayon FC. Ninashangaa kuambiwa na TFF kwamba ITC ya Kwizera ilishatumwa Rwanda," amesema Banda.
0 comments:
Post a Comment