Thursday, January 29, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kocha Mkuu wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic amekitoa kikosi chake katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) baada ya kuwa na matokeo hafifu katika mechi za mwanzo.

Simba SC imeshinda mechi mbili tu katika mechi 11 ilizocheza hadi sasa msimu huu, ikitoka sare mara saba na kupoteza mbili dhidi ya Kagera Sugar FC na Mbeya City FC.

Kutokana na matokeo hayo mabovu, Kopunovic ameweka wazi kwamba Simba SC haiwezi kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu.

Katika mahojiano na waandishi wa habari mara tu baada ya kumalizika kwa mechi yao ya jana waliyogongwa nyundo 2-1 na Wagonga Nyundo wa Mbeya, timu ya Mbeya City, Kopunovic alisema timu yake isitarajie ubingwa msimu huu kwa imejaa vijana ambao wanafanya makosa madogomadogo mara kwa mara kutokana na kukosa uzoefu.   

Alisema baada ya mechi hiyo kwamba kama Simba SC wana ndoto za ubingwa msimu huu, basi ajira yake iko hatarini kwa vile naye pia watamfukuza kama ilivyotokea kwa watangulize wake katika klabu hiyo iliyoanzishwa1936.

"Tuko kikosi kizuri kwa misimu ijayo, si msimu huu. Huwezi kusema uko kwenye mbio za ubingwa wakati kikosi kinafanya makosa yanayojirudia mara kwa mara.

"Tuna wachezaji wengi ambao ni vijana, hawana uzoefu mkubwa ndiyo maana wanafanya makosa hayo. Tukiwapa muda na sisi makocha tukavumiliwa, tutajenga kikosi imara kwa ajili ya kusaka ubingwa msimu ujao.

"Tuna wachezaji wengi wenye vipaji kikosini lakini wanahitaji muda. Tukitaka matokeo mazuri ya haraka, haitakuwa jambo jema kwetu maana mimi nimekabidhiwa timu muda si mrefu," alisema zaidi kocha huyo aliyesaini mkataba wa miezi sita kuinoa Simba SC siku ya Mwaka Mpya.

Kipigo cha jana kilikuwa cha kwanza kwa kocha huyo Simba SC, aliyeiongoza timu hiyo ya Msimbazi katika mechi nane, tano za Kombe la Mapinduzi na tatu za VPL. Mserbia huyo ameshinda mechi moja ya VPL dhidi ya Ndanda FC, sare moja dhidi ya Azam FC na kupoteza moja dhidi ya kikosi cha KOcha Bora wa msimu uliopita, Juma Mweambusi jana.

Kikosi hicho sasa kiko nafasi ya 10 katika msimamo wa VPL kikiwa na pointi 13, nane nyuma ya vinara Azam FC na mwishoni mwa wiki kitakuwa na kibarua kigumu mbele ya maafande wa JKT Ruvu Stars Uwanja wa Tafa jijini hapa.

Timu ya kocha mzawa Felix Minziro kiliizaba Simba SC mabao 3-2 katika mechi yao ya mwisho Uwanja wa Taifa msimu uliopita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video