Monday, January 26, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
Kama mashabiki wa Simba SC walifikiri Goran Kopunovic ndiye suluhisho la ukame wa ushindi kwao, walikuwa wanajidanganya! Kwa nini? Tega sikio...

Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema hajaja nchini na miujiza ya kuipa ushindi kila mechi timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.

Goran alitoa kauli hiyo katika mahoajino maalum kituo cha redio cha Clouds FM cha Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mechi yao ya raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) waliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifra jijini Dar es Salaam jana.

Kocha huyo aliyesaini mkataba wa miezi sita kuinoa Simba SC siku ya Mwaka Mpya akirithi mikoba ya Mzambia Patrick Phiri aliyetimuliwa, alisema ni vigumu kwake kwa sasa kuahidi kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu kwa kuwa kikosi chake bado kina upungufu mkubwa.

Goran amewataka viongozi, wanachama na mashabiki wa Simba SC kumpa muda zaidi wa kukitengeneza kikosi chao kwa kuwa amebaini hakikuandiliwa vyema kwa ajili ya msimu huu.

"Mpira wa miguu unahitaji maandalizi ya kutosha, kuna makosa kwenye timu yangu nimebaini yalifanyika wakati wa maandalizi ya msimu huu. Unapokosea katika wiki nane za maandalizi ya msimu ni tatizo kubwa.

"Timu yangu imefanya maandalizi makubwa kabla ya mechi hii, inashangaza kuona wachezaji wanashindwa kufuata nilichowaelekeza na kufikia hatua ya kushindwa hata kukimbia uwanjani.

"Mchezaji wa Ligi Kuu anakata pumzi anatembea, ni tatizo kubwa. Mimi si mchawi, sijaja na miujiza ya kuifanya Simba ishinde kila mechi. 

"Tumekutana na mabingwa watetezi, Azam ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri, tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kupata pointi moja dhidi ya timu ngumu kama hii. Ninaamini tutaendelea kuimarika na kufanya vizuri lakini siwezi kuahidi kwamba Simba itatwaa ubingwa msimu huu," alisema Goran.

Simba SC iko nafasi ya 10 katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi 13, nane nyuma ya vinara Azam FC na nne mbele ya Tanzania Prisons wanaokamata mkia. Nafasi ya pili inakaliwa na Yanga SC wenye pointi 18, moja nyuma ya JKT Ruvu Stars katika nafasi ya tatu walifuatwa na Mtibwa Sugar FC wenye pointi 17, Coasta Union FC wenye pointi 16 na Polisi Moro wenye pointi 15 katika nafasi za nne, tano na sita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video