Wednesday, January 14, 2015

Goran na Ivo Mapunda walikumbatiana kwa muda mrefu baada ya kutwaa ubingwa

KOCHA mkuu wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic amesema kipa wake Ivo Mapunda ni shujaa mkubwa na uzoefu wake unaisaidia timu.
Kopunovic aliuambia mtandao huu baada ya kipa huyo kudaka penalti ya mwisho ya Vicent Barnabas wa Mtibwa na kuwapa Ubingwa Simba kuwa aliamua kufanya mabadiliko ya kumtoa Peter Manyika ‘Junior’ na kumuingiza Ivo kwasababu ya uzoefu.

“Ivo ni kipa mzoefu sana, ndio maana nilimuingiza, angalia alichofanya, nimefurahi sana na imetupa morali kubwa”

Kocha huyo amewapongeza wachezaji wake kwa kupigana mwanzo mpaka mwisho ingawa hawajakaa naye kwa muda mrefu.


“Tumechukua Mapinduzi, lakini malengo yetu ni ligi kuu. Kweli mechi hii ilikuwa muhimu sana, ila ligi ni muhimu zaidi”. Alisema Kopunovic.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video