Monday, January 26, 2015


KOCHA wa Zambia, Honour Janza amesema hategemei bahati kuvuna pointi tatu dhidi ya Cape Verde katika mechi ya mwisho ya kundi B kuwania kufuzu robo fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2015.
Cape Verde ambao wapo nafasi ya pili wakijikusanyia pointi mbili sawa na DR Congo, wanakabiliana na Zambia wanaoshika mkia wakiwa na pointi moja wakati Tunisia wanaongoza kwa pointi tatu.
Zambia na Cape Verde wanafahamiana vizuri kufuatia kukutana mapema katika kampeni ya kuwania kufuzu Afcon 2015.
"Jambo zuri ni kwamba tunafahamiana. Cape Verde wanatujua na sisi tunawajua wao," Amesema Janza.
"Kwahiyo nadhani itakuwa mechi ya mvuto na timu nzuri itashinda lakini sio bahati".
"Hatuhitaji kingine zaidi ya ushindi".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video