Kocha msaidizi wa klabu ya Real Madrid
Paul Clement amesema Winga wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale hataondoka
katika klabu hiyo siku za hivi karibuni kwani bado wanamuitaji mchezaji huyo
kwa udi na uvumba kwa ajili ya kuisaidia klabu hiyo kutwa mataji mbalimbali
barani ulaya likiwemo lile la klabu bingwa Barani Ulaya.
Bale ambaye alikuwa anahusishwa na kutimkia katika klabu ya Manchester United
alijiunga na Real Madrid kwa kitita cha Pauni 100M kutoka Tottenham Hotspurs
mwaka 2013, ameisaidia klabu klabu hiyo kutwaa ubingwa wa klabu bingwa Barani Ulaya lakini pia kombe la Mfalme Copa delay akishirikiana na mshambuliaji
machachari wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo.
Clement alisema hajui taarifa hizo zimetoka wapi kuwa
Bale anaondoka katika dimba la Santiago Bernabeu wakati Winga huyo mwenye umri
wa miaka 24 anaumuhimu mkubwa sana katika klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment