Mrisho Ngassa |
KOCHA mkuu wa Yanga SC, Mholanzi, Johannes Hans
van der Pluijm anaamini Mrisho Ngassa atarudi katika kiwango chake cha zamani.
Pluijm alikiri wazi kuwa nyota huyo ameshuka kiwango
kwa sasa na ndio maana anaanzia benchi
katika mechi mbalimbali, lakini anaonesha juhudi kubwa mazoezini kitendo
kinachoonesha wazi ametambua alipo sasa.
“Kiwango cha Ngassa kimeshuka, lakini ni
mchezaji mwenye akili, lazima atarudi katika kiwango chake”. Alisema Pluijm.
Kocha huyo anayependa soka la kushambulia
aliongeza kuwa kwasasa kikosi chake kimesheheni nyota wa kiwango cha juu, hivyo
inawalazimu wachezaji kufanya jitihada za kumshawishi.
Moja kati ya mechi kubwa ambayo Ngassa hakuanza chini
ya Pluijm mwishoni mwa mwaka jana ni ile ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi
ya Azam fc iliyopigwa desemba 28 mwaka jana uwanja wa Taifa ambapo timu hizo
zilitoka sare ya 2-2.
Katika mechi hiyo, Ngassa alichezeshwa dakika 7 tu
kitendo kilishoashiria mchezaji huyo kipenzi kwa Wana Yanga si mchezaji tegemeo
tena katika kikosi cha Yanga.
Kocha huyo aliongeza kuwa siku zote anapenda kucheza
mpira wa wazi, akishambulia zaidi kwa lengo la kufunga magoli mengi, hivyo
nguvu zake zipo katika kuwanoa viongo wake na washambuliaji wake.
Kwasasa Pulijm anapenda kuwatumia zaidi Kpah
Sherman, Danny Mrwanda, Amissi Tambwe, Saimon Msuva, Andrey Coutinho katika
safu ya ushambuliaji, huku Ngassa, Hussein Javu wakianzia benchi.
0 comments:
Post a Comment