Steven Mazanda |
KIUNGO mahiri wa Mbeya City fc, Steven Mazanda
amesema wapo katika hali nzuri kuelekea mechi ya kesho ya ligi kuu Tanzania
bara dhidi ya Polisi Morogoro itayopigwa uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mazanda ameuambia mtandao huu muda huu kwa njia ya
simu kutoka mji kasoro bahari kuwa hawezi kuwaogopa Polisi.
“Mpira ni kazi yangu, nitawaogopaje Polisi?, tuko
vizuri kwa ajili ya mechi”. Amesema Mazanda.
Kiungo huyo mwenye ufundi mwingi amesema wamepita
wakati mgumu, lakini siri ya kurejesha makali ni kujituma na kukubali kukosea,
halafu kujifunza upya.
Mazanda aliyekuwepo katika kikosi cha kwanza kilichoifunga
Simba mabao 2-1 katikati ya wiki hii (januari 28 mwaka huu) amesema wapinzani
hao waliochanganyikiwa na kipigo inabidi wakubali changamoto na kujipanga upya.
“Wavumilie, mpira ndivyo ulivyo. Hata sisi
tulipita wakati wa mpito”. Amesema Mkongwe huyo aliyepachikwa jina la ‘Babu’.
0 comments:
Post a Comment