Inaaminika Cristiano Ronaldo amethibitisha kuachana na Irina Shayk
SIRI imefichuka!. Cristiano Ronaldo alisherehekea mwaka mpya peke yake baada ya mchumba wake, Mrusi kutokwenda katika sherehe ya siri aliyoandaa nyumbani kwao Madeira, gazeti maarufu la Ureno la Correio da Manha rimeripoti.
Gazeti hilo limetoa habari jana na kuthibitisha kuwa familia ya Ronaldo imevunjika baada kukosekana kwa maelewano baina ya Ronaldo na mpenzi wake Irina.
Irina mwenye miaka 29 alituma ujumbe kuwa amejiondoa katika wafuasi wa Ronaldo katika mtandao wa Twite ambaye ni mpenzi wake wa miaka mitano.
Drama hiyo ilianza baada ya Irina kushindwa kuhudhuria sherehe za tuzo za Ballon d'Or mjini Zurich siku ya jumatatu.
Cristiano mwenye miaka 29 aliungana na mtoto wake wa kiume mwenye miaka minne, Cristiano Jr jukwaani baada ya kupewa tuzo yake ya tatu ya mwanasoka bora wa dunia.
Katika hotuba yake aliishukuru familia yake, wachezaji wenzake na mashabiki wake, lakini hakumtaja mchumba wake Irina.
Ronaldo na Irina mwaka 2011
Baadaye ripoti zilieleza kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid amevunja mahusiano na mwanamitindo huyo wa Urusi baada ya kugoma kuacha kazi yake na kuwa mke na mama wa nyumbani.
Vyanzo vya karibu na mwanasoka huyo wa Ureno vimelieleza gazeti la Ureno la Correio da Manha kuwa mgogoro huo ulianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Ronaldo, Dolere wakati wapenzi hao walipokuwa katika mapumziko ya Krismas mjini Dubai.
Vyanzo vilisema: "Cristiano alitaka kumfanyia mama yake 'sapraizi na alifurahia krismas na Irina huko Dubai, alipanga kuwa naye katika sherehe ya kuzaliwa ya mama yake, lakini Irina hakutaka kwenda".
"Suala hilo lilileta mgogoro mkubwa na kusababisha kila mtu kufurahia sherehe za mwaka mpya peke yake na hawajawa na mahusiano mazuri miezi michache iliyopita".
Gazeti hilo pia limedai kuwa Irina aliamua kukaa hotelini kwenye moja ya ziara zake Madrid kwasababu Doleres alipigwa picha akitoa machozi akiwa katika nyumba ya kifahari ya Ronaldo huko VIP estate La Finca kufuatia mwanaye kushinda tuzo ya tatu ya Ballon d'Or.
“Dolores anaamini Irina hakuwa mwanamke sahihi kwa mtoto wa Ronaldo,” vyanzo vililiambia gazeti la Correio da Manha.
Irina na Cristiano, ambao walianza mahusiano baada ya kukutana Armani Photoshoot hawajathibitisha taarifa hizo rasmi za kuachana.
Msemaji wa Irina amedai kuwa mwanamitindo huyo alishindwa kuhudhuria Ballon d'Or kwasababu alikuwa na majukumu mengine.
0 comments:
Post a Comment