Saturday, January 24, 2015

KIJANA mpole ambaye hapendi makuu wala kuzungumzia mambo ya mpira akiwa likizo, Hassan Suleiman Isihaka  ameteuliwa kuwa nahodha wa timu ya Simba akisaidiwa na Jonas Mkude.
Isihaka ambaye hupendelea zaidi mtandao wa kijamii wa Watsup ‘kuchati’ na marafiki zake ameteuliwa jana  na kocha mkuu wa klabu hiyo, Mserbia Goran Kopunovic baada ya mazoezi ya muda mfupi uwanja wa Boko Veteran.

Hata hivyo kocha huyo ameteua wachezaji wakongwe ambao watakuwa wanawashauri pale yanapohitajika maamuzi ya busara.

Wachezaji hao ni Ivo Mapunda, Shaaban Kisiga, Masoud Nassor ‘Cholo’ na Mganda Emmanuel Okwi.


Isihaka alianza kuiongoza Simba katika michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo klabu hiyo ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Mtibwa Sugar Penalti 4-3 katika mechi ya fainali iliyopigwa januari 13.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video