Tuesday, January 6, 2015

SAM_4331
Wachezaji wa Simba, kutoka kulia, Jonas Mkude, Ramadhani Singano 'Messi', Elius Maguli, Said Ndemla na Danny Sserunkuma wakijiandaa kuanza mechi jana usiku

BEKI wa kulia wa Simba, Hassan Ramadhan Kessy amewataka Wanasimba wote kuiunga mkono timu yao ili kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu.

Kessy aliuambia mtandao huu jana usiku baada ya Simba kushinda bao 1-0 dhidi ya JKU na kufuzu robo fainali ya kombe la Mapinduzi kuwa;

‘Simba ni timu yetu wote. Umoja utatupatia mafanikio. Niwaambie mashabiki wa Simba, hii ni timu yetu, tusitengane”. Alisema Kessy.

Beki huyo anayepanda na kushambulia kupitia winga ya kulia aliongeza kuwa kocha mpya amekuja, mbinu zake ni nzuri, kinachotakiwa na kumpa muda ili atimize malengo ya timu.

Kessy aliyesajiliwa na Simba wakati wa dirisha dogo mwezi desemba mwaka jana akitokea Mtibwa Sugar alikuwa na uhakika wa namba katika kikosi cha Patrick Phiri.

Alicheza kwa mara ya kwanza  katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mwadui fc uwanja wa Taifa Dar es salaam, akakipiga dhidi ya Taifa ya Jang’ombe uwanja wa Amaan Zanzibar(mechi ya kirafiki) na akacheza mechi ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, mechi iliyomfukuzisha kazi Phiri baada ya kulala kwa bao 1-0.


Katika michuano ya Mapinduzi inayoendelea visiwani hapa, beki huyo amecheza mechi zote tatu , moja chini ya Seleman Matola dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Mnyama alipigwa 1-0 na mechi mbili dhidi ya Mafunzo na JKU chini ya Goran Kopunovic, Simba ikishinda zote kwa bao 1-0.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video