Tuesday, January 6, 2015


SAM_4345
Na Bertha Lumala
KCCA FC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uganda, wameifumua mabao 2-1 timu ya KMKM katika mechi yao ya mwisho ya Kundi B la Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan, Zanziba jioni hii.

KCCA waliokianza kwa kasi kipindi cha pili, wamefanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na kiungo mshambuliaji Herman Waswa akimalizia krosi maridhawa ya Dilungi Michael dakika ya 47.

Hilo lilikuwa goli la pili kwa mfungaji huyo wa bao lililoipa KCCA ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mwaka jana kwani alifunga pia goli la kwanza katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mtende mwishoni mwa wiki.

Dakika ya 82 KMKM walifanya kazi nzuri na kupata bao la kusawazisha kupitia Mwinyi Haji kwa shuti kali la faulo lilokwenda moja kwa moja langoni.

Hata hivyo, dakika mbili baadaye KCCA wakafanya shambulizi la kushtukiza na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa mpikaji wa bao la kwanza, Dilungi ambaye alipiga shuti kali la mguu wa kulia nje kidogo mwa boksi.
 
Kwa mujibu wa Azam TV wanaorusha maja kwa moja matangazo ya michuano hiyo, KMKM walipata kona tatu dhidi ya tano za KCCA huku timu hiyo ya Zanzibar ikimiliki mpira kwa asilimia 48 dhidi ya 52 za wageni.

POLISI 0-0 TAIFA
Kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung visiwani hapa, Polisi Zanzibar na Taifa ya Jang'ombe zimetoka suluhu katika mechi ya mwisho ya Kundi A.

Matokea hayo yameifanya Yanga imalize kileleni mwa kundi hilo ikifuatwa na timu hizo mbili ambazo zote zina pointi nne zikifanana kwa kila kitu huku Chama cha Soka Zanzibar na Kamati ya Mashindano hayo wakiamua kurusaha sarafu kumpata mshindi wa pili kati ya timu hizo. 

Vikosi vilikuwa;
Mugabi Yasin, Mpiama Saka, Namwanya Simon, Kiseka Ronnie, Kizza Ibrahim, Mtege Ivan, Dilungi Michael, Owen Kasule, Waswa Herman, Mucureezi Paul/ Lukwiya Rogers (dk 72) na Wadri William.

KMKM: Mudathir Khamis, Kassim Abdulkadir, Mwinyi Haji, Idd Mgenzi, Khamis Ali, Ibrahim Khamis, Nassor Ali, Khalid Kheri, Tizzo Chomba/ Haitham Hamis dk 81, Fakih Mwalim na Mudrik Muhibu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video