WAGONGA nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc wameanza kurejesha makali yao baada ya kuitandika bao 1-0 Kagera Sugar katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Bao hilo pekee limefungwa dakika ya 80 na Peter
Mapunda.
Kikosi hicho cha Juma Mwambusi kilishangiliwa na
zaidi ya mashabiki 200 waliosafiri kutoka Mbeya kuipa sapoti timu hiyo.
Ushindi wa huu ni wapili mfululizo kwani desemba
28 mwaka jana waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda fc katika mechi
ya raundi ya nane ya ligi kuu kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Mbali na Kirumba, Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga
ulikuwa na kibarua cha kuhimili daluga za maafane wawili, Mgambo JKT dhidi ya
Tanzania Prisons katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyocheza jioni
ya leo.
Mechi hiyo imemalizika kwa timu zote kutoka suluhu
(0-0).
0 comments:
Post a Comment