Monday, January 5, 2015

11Mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Azam FC amesema timu za Yanga, Mtibwa Sugar na KCCA ya Uganda ndizo ziwapa wakati mgumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwaka huu.
Baada ya kumalizika kwa mechi yao ya pili ya Kundi B waliyoshinda kwa bao 1-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar KMKM kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa jana usiku, Kavumbagu alisema timu hizo zinatisha.
“Yanga, KCCA na Mtibwa wako vizuri, si timu za kutamani ukutane nazo katika michuano hii. Yanga wameimarika, Mtibwa bado wako katika kiwango chao cha Ligi Kuu. Hii timu kutoka Uganda inacheza kwa ushirikiano sana,” alisema Kavumbagu.
Kavumbagu, ambaye alikosa mechi mbili za mwanzo za Kundi B kutokana na ugonjwa wa tyford unaomsumbua, alisema anatarajia kurejea kesho katika mechi yao ya mwisho ya kundin hilo dhidi ya Mtende kwenye Uwanja wa Amaan saa 9:00 mchana.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video