NAHODHA wa Mbeya City fc Mwengane
Yeya amesema kikosi cha nyota 11 waliokuwepo uwanjani kwenye mchezo wa ligu kuu
ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba-Mwanza
walicheza vizuri na kwa kiwango bora jambo lililochangia Mbeya City Fc kuibuka
na ushindi wa bao 1-0.
Akizungumza na Tovuti rasmi ya
klabu hiyo mara baada ya mchezo kumalizika jana jioni, Yeya aliyekuwa kwenye
orodha ya wachezaji wa akiba alisema kuwa nidhamu ya hali ya juu uliyooneshwa
na wachezaji wote waliokuwa uwanjani na waliokuwa kwenye bechi imesababisha
kupatikana kwa ushindi huo kufuatia ushirikiano mkubwa uliouwepo.
“Hakika timu imecheza vizuri,
kulikuwa na ushirikiano mkubwa kati yao, zaidi walikuwa na nidhamu ya hali ya
juu ndiyo maana umeona kuna wakati mwamuzi alikuwa anatoa maamuzi ya utata
lakini hawakuliangalia hilo walibaki mchezoni wakajituma muda wote nasi
tuliokuwa benchi tuliwapa sapoti, hili limenifurahisha sana, tunashukuru kupata
pointi tatu ugenini hii ni hamasa ya kupata tatu zingine kwenye mchezo
unaofuata ambao tutacheza nyumbani” Yeya amekaririwa na Tovuti ya klabu.
0 comments:
Post a Comment