Baada ya Uongozi wa Klabu ya Yanga kutangaza kuachana na aliekuwa mlindamlango wake Juma Kaseja na baadae kumfungulia mashtaka katika Mahakama ya kazi , hatimaye mlind amlango huyo sasa anatarajia kusomewa mashtaka yanayomkabili February 12 mwaka huu.
Hatua hiyo ilikuja kufuatia Kaseja kudai alipwe fedha zake za usajili zilizokuwa zimesalia na kutaka kuvunja mkataba wake , lakini baadae Klabu hiyo ilimuingizia pesa hizo katika akaunti yake bila kumpa taarifa na kupelekea kuwepo kwa mgogoro baina ya pande hizo mbili.
Mkuu wa Idara ya Sheria ya Klabu hiyo FRANK CHACHA ameiambia mtandao huu kwamba wamepokea samasi inayomtaka mlindamlango huyo kufika Mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo.
0 comments:
Post a Comment