Gareth Bale akihojiana na redio ya Hispania ya Cadena Ser
Gareth Bale amesema wana mahusiano mazuri sana na Cristiano Ronaldo
MCHEZAJI ghali zaidi duniani, Gareth Bale amekanusha tetesi za kujiunga na Manchester United na amesisitiza kuwa uhusiano wake na mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ni mzuri na haijawahi kutokea.
Mshambulizi huyo amesema bado amebakiza miaka mingi katika mkataba wake Madrid na amekanusha tetesi kuwa hana furaha katika mji mkuu wa Hispania, Madrid.
Bale amezungumza na redio Cadena SER katika shoo ya 'El Larguero' jana usiku.
0 comments:
Post a Comment