WAKATA miwa wa
Kaitaba, Kagera Sugar FC wamesema sasa wameiva kuivaa Azam fc katika mchezo wa
kiporo wa ligi kuu soka Tanzania bara utakaopigwa kesho (januari 20) uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza.
Kocha msaidizi wa ‘Wanankurukumbi’
hao, Murage Kabange amesema baada ya kutandikwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City
jumamosi iliyopita, hawatakubali kuacha pointi tatu kwa mara nyingine mbele ya
mabingwa watetezi.
“Tumejipanga,
tumezungumza na vijana, tumewajenga kiakili na muda wote asubuhi tumefanya
mazoezi mepesi, tuna matumaini kwamba kesho tutfanya vizuri katika mchezo huo
ambao utakuwa mgumu kwasababu wenzetu walikotoka wamepata matokeo, kwahiyo
wamekuja na nguvu ya kupata pointi tatu ambazo ni muhimu kwao”. Amesema Kabange
katika mahojiano na mtandao huu. Aliongeza. “Tulipoteza mechi, lakini si kweli
kwamba ukipoteza mechi basi kunakuwa na matatizo, naweza kusema hatukuwa na
bahati kwasababu sikuona nini ambacho wenzetu walituzidi zaidi ya nafasi ile
moja waliyoipata na kufunga goli dakika ya 80”.
Wakati huo huo Azam
fc wamefanya mazoezi asubuhi uwanja wa CCM Kirumba kuweka miili sawa kabla ya
mechi ya kesho.
Meneja wa klabu hiyo,
Jemedari Said Mzumari amesema wamekusudia kuchukua pointi sita kanda ya Ziwa na
kumalizia za Simba Dar es salaam, kisha kwenda Lubumbashi, DR Congo tayari kwa maandalizi ya ligi ya
mabingwa.
Azam waliibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Stand United katika mechi ya ligi kuu
iliyopigwa jumamosi uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment