KIONGOZI wa tawi la Mpira Pesa la Magomeni jijini
Dar es salaam, Ustadh Masoud kwa niaba ya wanachama wenzake amemshutumu makamu
wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kuhusika katika matokeo mabaya ya
klabu hiyo katika mechi za ligi kuu Tanzania bara.
Masoud amezungumza leo kuwa wamepata taarifa kuwa
Kaburu analipangia benchi la ufundi wachezaji wa kucheza.
“Tumesikia kuwa kiongozi wa juu (Kaburu) anahusika
kupanga wachezaji, hii haiwezekani, tukikutana tutajadili hili na kuchukua
hatua”. Alisema Masoud.
Alipotafutwa Kaburu amekanusha taarifa hizo na
kudai kiongozi huyo lazima aangaliwe sana kwani ana nia mbaya ya kuivuruga
klabu.
“Nimemsikia akisema Kaburu anahusika kupanga
wachezaji, binafsi nakanusha hilo, uongozi tutamchukulia hatua kwa kumpeleka
kamati ya maadili ya klabu”. Amesema Kaburu.
0 comments:
Post a Comment