
Jose Mourinho amesema itakuwa aibu kufunwa na Bradford
JOSE Mourinho amesema itakuwa ni aibu kama leo Chelsea itafungwa na Bradford katika mechi ya raundi ya nne ya kombe la FA.
Katika siku nne, Chelsea wana mechi mbili za makombe ikiwemo mechi ya marudiano ya nusu fainali ya kombe la ligi itayopigwa jumanne ijayo dhidi ya Liverpool.
Lakini meneja wa 'The Blues' amesisitiza kuwa leo anachezesha kikosi imara licha ya kuwapumzisha John Terry, Thibaut Courtois na Diego Costa.
"Ili kuwepo kwenye mbio za ubingwa kitu kizuri ni kupoteza mechi dhidi ya Bradford, Liverpool na Paris Saint-Germain (mechi ya ligi ya mabingwa) na ubaki kucheza ligi kuu tu mpaka mwisho wa msimu", Alisema Mourinho.

Chelsea watakuwa wenyeji wa Bradford, ambao waliwafunga Millwall katika mechi ya marudiano ya raundi ya tatu.
"Haya ni mazingira kamili. Lakini sio kwetu, sio kwa Chelsea.
"Kuna siku moja kocha wa timu kubwa alitolewa kwenye kombe na alisema, "Vizuri, sasa tunaweza kujikita zaidi kwenye mashindano mengine". Kama nitapoteza dhidi ya Bradford sitasema hivyo. Nasema, "Itakuwa aibu."
0 comments:
Post a Comment