Monday, January 5, 2015

MABINGWA mara mbili mfululizo wa Tanzania mwaka 1999 na 2000, Mtibwa Sugar wametoka suluhu pacha ya bila kufungana na Mafunzo ya Zanzibar katika mechi ya mwisho ya kundi C iliyomalizika jioni hii uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mtibwa Sugar wamefikisha pointi tano kufuatia kushinda mechi moja na kutoka sare mbili.

Mafunzo wao wameshatupwa nje ya mashindano baada ya kuambulia pointi moja katika mechi tatu ambapo ilichapwa mara na kutoka sare mechi moja.

Mechi ya kwanza Mafunzo walotandikwa  2-0 na JKU, mechi ya pili wakafungwa bao 1-0 na Simba na leo wameambulia sare.


Usiku majira ya saa 2:15, Mnyama Simba atachuana na JKU katika uwanja wa Amaan kukamilisha mechi ya hatua ya makundi.

Kama Simba watashinda mechi hiyo watafikisha pointi 7 kibindoni na kuibuka vinara wa kundi hilo.

Kama timu hizo zitatoka suluhu au magoli, basi Simba watashika nafasi ya tatu kwa kujikusanyia pointi nne, wakati JKU watakuwa vinara kwa pointi tano sawa na Mtibwa katika nafasi ya pili, lakini tofauti ni magoli ya kufunga na kufungwa.

Mpaka sasa Mtibwa wameshafunga magoli mawili na kufungwa moja, wakati JKU wamefunga magoli matatu na kufungwa moja.

Kwa mujibu wa ratiba kama Simba watakuwa wa tatu kwa maana ya mshindwa bora watachuana na vinara wa kundi A ambao ni Yanga.

Tayari joto limeshaanza kupanda kwa mashabiki kwani kuna dalili kubwa ya watani kukutana katika hatua ya robo fainali.



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video