JKT Ruvu Stars imejipanga kuichapa Simba na kuizidishia
machungu zaidi katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara itayopigwa kesho jioni
uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Fredy Felix Minziro
amesema wanafahamu wazi kuwa Simba wamejeruhiwa, lakini vijana wake wapo tayari
kucheza soka maridadi kabisa.
“Naomba mashabiki waje kwa
wingi kuona soka la burudani ambalo hawajaliona kwa siku nyingi, tunatambua
Simba wamejeruhiwa, lakini nawaambie waje kucheza mpira na wasije na vitendo
vya kihuni”. Amesema Minziro
0 comments:
Post a Comment