Klabu ya Manchester United inatarajiwa
kuchuana vikali na Leicester katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford,huku klabu hiyo ikiendelea kukumbwa na wimbi la majeruhi ambapo kiungo
wa kati Michael Carrick hatocheza katika mechi
yoyote kwa kipindi cha wiki tatu baada ya kupata jeraha la misuli.
Ashley
Young anakaribia kupona jeraha baada ya kuumia nyuma ya goti lake,huku
Jonny Evans na Chris Smalling wakitarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi.
Mathew Upson
huenda akarejea tena katika kikosi cha kwanza cha Leicester baada ya
kupona jereha la goti alilopata kabla ya msimu kuanza.
Matty James yupo nje kwa kadi nyekundu,Riyad Mahrez bado yuko Afrika akiichezea timu ya Taifa yake ya Algeria huku Kasper Schmeichel na Chris Wood wakiwa bado
wako nje kwa majeraha.
0 comments:
Post a Comment