Nahodha Yaya Toure ataiokoa Ivory Coast
IVORY Coast leo majira ya saa 3:00 usiku inatarajia kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Cameroon katika michuano ya mataifa ya Afrika, Afcon 2015 inayoendelea huko Guinea ya Ikweta mbele ya Cameroon.
Timu zote za Kundi D (Mali, Ivory Coast, Cameroon, Guinea) hazijapata ushindi na zinafungana kwa pointi mbili mbili kufuatia sare ya 1-1 na mechi zao za mwisho wanahitaji ushindi dhidi ya miamba hii ya Afrika.
Ingawa Tembo wanaingia uwanjani bila mshambuliaji Gervinho ambaye alioneshwa kadi nyekundu katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Guinea, Max Gradel anatarajia kutatua ukame wa magoli kwa Tembo hao wa Pwani ya magharibi wa Africa.
Kwa upande wa Simba wasiofugika, Cameroon nao wanahitaji njia ya kupenya mbele ya safu ya ulinzi ya Tembo inayoongozwa na Kolo Toure na Siaka Tiene ili kupata pointi tatu zitazowapeleka robo fainali.
Mechi nyingine itayoanza muda huo huo itawakutanisha Mali dhidi ya Guinea.
Timu hizi pia zinafungana kwa pointi mbili.
Kundi D timu zote zinalingana kwa kila kitu, hivyo timu yoyote itakayoshinda itafuzu .
Kama timu zote zitatoka sare inayofanana kama huko nyuma, kanuni itabidi zitumike.
RATIBA
21:00
? - ?
21:00
? - ?
0 comments:
Post a Comment