Thursday, January 15, 2015

KIPA Ivo Mapunda hivi karibuni alitangaza kutoichezea Simba katika mechi zozote kwa kuwa kila anapofungwa analaumiwa.
Lakini akiwashangaza wengi, juzi Jumanne usiku katika fainali ya Kombe la Mapinduzi aliingia uwanjani katika dakika ya 90 na kupangua penalti moja iliyoipa ubingwa timu yake.
Baada ya mechi hiyo, Mapunda aliliambia Mwanaspoti kuwa alishindwa kukataa kuingia kuchukua nafasi ya Manyika Peter kwani Kocha Goran Kopunovic alimshtukiza kumpa nafasi hiyo na hakuweza kukataa kutokana na hali halisi.
Baada ya kuona mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar inaelekea katika mikwaju ya penalti, Kopunovic alimwingiza Mapunda ambaye alifanikiwa kupangua penalti ya mwisho ya Vincent Barnabas na kuipa Simba ushindi wa penalti 4-3.
“Kweli nilisema sitaichezea tena Simba baada ya maneno kuwa mengi kwamba nafungisha, nilicheza na Mtibwa kwa sababu kilikuwa kitu cha ghafla ambacho kocha aliniambia nami nikajikuta nimesimama na kwenda uwanjani,” alisema.
“Kweli kama ningefanya vibaya pale hali ingekuwa mbaya zaidi, ningeonekana nimefungisha, lakini namshukuru Mungu.”
Alipoulizwa kama msimamo wake bado uko palepale, Mapunda alishindwa kufafanua zaidi.
Mapunda hakucheza mechi yoyote ya michuano hiyo awali na ameweka rekodi ya kipa aliyecheza kwa muda mfupi michuano hiyo.
Akizungumzia uhodari wake wa katika penalti, Mapunda alisema alimchanganya kisaikolojia kiungo wa Mtibwa Sugar, Ibrahim Rajabu ‘Jeba’, kwa kutompa mpira uliokuwa wavuni. “Mpira una mambo mengi, nilifanya makusudi kutompa mpira Jeba kwa lengo la kumtoa mchezoni, kweli alitoka mchezoni ndiyo maana alikosa penalti kwa kugongesha mwamba.”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video