Wednesday, January 14, 2015

MKOMBOZI wa Simba katika mechi ya fainali ya kombe la Mapinduzi iliyopigwa uwanja wa Amaan usiku huu, Mjini Zanzibar, Ivo Philip Mapundo amejawa na furaha kubwa baada ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa kufuatia kudaka penalti ya Vicent Barnabas iliyowapa ushindi.
Akizungumza kwa furaha na mtandao huu baada ya mechi kumalizika Ivo alisema: “Mwalimu aliniamini, akaniingiza dakika za majeruhi kwa lengo la kudaka penalti. Kitu cha kwanza nilichowaza ni kutokumuangusha mwalimu. Kwali nimefanya vizuri, nina furaha sana”.


Kipa huyo alisema katika siku tatu alizofanya mazoezi, mwalimu alimuona katika mazoezi ya kudaka penalti na akamwambia kuwa kama itafikia hatua ya matatu angemtumia.

Pia amewataka wanasimba kuwa na umoja katika kipindi hiki kizuri kwani kuwa na migongano kutaishusha timu.


“Kikubwa wanasimba wawe na subiri, timu ni nzuri na tunaamini tutafanya vizuri katika mechi za ligi”. Aliongeza Ivo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video