Thursday, January 8, 2015

Isihaka (kulia) akiwa katika majukumu yake kwenye moja ya mechi ya kombe la Mapinduzi

NAHODHA wa Simba, Hassan Suleiman Isihaka amesifu mbinu mpya za kocha Goran Kopunovic ambaye ameshinda mechi zote tatu za kombe la Mapinduzi akikalia benchi la ufundi.

Simba chini ya kocha Msaidizi Seleman Matola ilipoteza mechi ya kwanza ya kombe la Mapinduzi kwa bao 1-0, ikiwa chini ya Kopunovic ilishinda goli 1-0 mara mbili dhidi ya Mafunzo na JKU na hapo jana ikashinda mabao 4-0 dhidi ya Taifa ya Jang’ombe hatua ya robo fainali.

Isihaka mwenye asili ya upole alisema Kopunovic anawafundisha zaidi kukaba kwa uangalifu na kushambuli muda wote.

“Kocha ana mbinu mpya. Timu inacheza vizuri, kila mchezaji ana morali kubwa. Sisi tunafanya kazi kama tulivyoagizwa na mwalimu, suala la ufundi na mbinu ni juu yake”. Alisema Isihaka.


Beki huyo alisema mashabiki wa Simba watarajie makubwa kutoka kwa vijana wa Simba kwani kocha ameonekana kufaa kwa vitu vingi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video