Wednesday, January 14, 2015

 Isihaka akiwa na kombe la Mapinduzi walilotwaa baada ya kuifunga Mtibwa Sugar

NAHODHA wa Simba, Hassan Suleiman Isihaka alikosa cha kuzungumza baada ya kuiongoza Simba kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi katika mechi ya fainali aliyopigwa uwanja wa Amaan Mjini Unguja ,Zanzibar.

Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu ya bila kufungana na hatimaye Simba kuibuka washindi kwa penalti 4-3, Isihaka alicheza safu ya ulinzi akisaidiana na Juuko Mursheed, huku kushoto akikaa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kulia Hassan Ramadhani Kessy.

“Sina cha kuzungumza zaidi, nimejawa na furaha kubwa mno. Nawashukuru mashabiki, wanachama, viongozi na wachezaji wenzangu kwa kufanya kazi hii kubwa”.


“Nachaguliwa kuwa nahodha wa Simba kwa mara ya kwanza halafu naiongoza timu kuchukua ubingwa, hakika nimefurahi sana” Alisema Isihaka.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video