
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger mwezi huu anaiwinda saini ya Gabrial Paulista kutoka Villarreal
UNAWEZA kusema mpango wa Arsenal kumsajili Gabriel Paulista mwezi huu wa januari umepata nguvu baada ya beki huyo mwenye thamani ya paundi milioni 15 kuachwa katika kikosi cha Villarreal kinachoivaa Levante wikiendi hii.
Villarreal walitangaza kikosi cha wachezaji 18 kinachochuana na Levante uwanja wa El Madrigal na waliorodhesha wachezaji watakaokosa mechi kwasababu ya majeruhi na kutumikia adhabu.
Japokuwa kuachwa kwa jina la Paulista, klabu haijatoa sababu katika tangazo lake, lakini inaripotiwa kuwa nyota huyo yuko njia kutimka.

Arsenal wanaweza kukumbana na kikwazo cha kupata kibali cha kazi kwa beki huyo raia wa Kibrazil
0 comments:
Post a Comment