Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, amepata malaria na huenda asicheze mechi ya Jumatatu dhidi ya Senegal.
Chama cha soka cha Ghana kimesema mshambuliaji huyo alilazwa katika hospitali mjini Mongomo siku ya Jumamosi na kuruhusiwa siku ya Jumapili.
Malaria hiyo ilikuwa katika hatua za mwanzo na Gyan anaendelea vizuri na matibabu.
Wakati huohuo meneja wa Senegal Alain Giresse inabidi afanye uamuzi kuhusu Sadio Mane ambaye ni majeruhi.
Mshambuliaji huyo wa Southampton alijumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa licha ya klabu yake kusisitiza kuwa mchezaji huyo hayuko tayari kucheza.
0 comments:
Post a Comment