Gwiji wa zamani
wa Arsenal, Mfaransa Thierry Henry ameanza kazi Sky Sports huku akidai timu
hiyo imeshuka kabla klabu yake hiyo haijaibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya
mabingwa watetezi Manchester City
Mapema kabla ya mchezo huo Henry mwenye miaka 37 sasa aliikosoa klabu hiyo huku
akisema inakosa kiungo wa ulinzi madhubuti wa kuwalinda Per Mertasacker na
Laurent Konscienly. Nyota huyo alidai mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ambaye
kwa sasa anatesa West Ham Alex Song angeweeza kumudu kuiboresha seehemu hiyo na
hivyo kukosekana kwa kiungo wa ulinzi kunaifanya kupitika kirahisi
Hata hivyo
washika bunduki hao walimudu kuibuka na ushindi wa bao 2-0 ugenini kupitia
mabao ya Santi Cazorla na Olivier Giroud
Nyota huyo,
alisisitiza na kukumbushia enzi za Patrick Vieira na Gilberto Silva ambao
waliiwezesha Arsenal kumaliza msimu pasipo kupoteza msimu wa 2003-04.
Nyota huyo
akaendelea kusisitiza kuwa ukiitizama timu hiyo ni kama yenye kupigania nne
bora pekee. Hata hivyo alisema ni wakati wa wao kupambana kuwania mataji. “nina
uhakika Arsene, washabiki na bodi haya wanataraji zaidi na zaidi. Inaweza
kusikitisha Arsenal kufungwa na Stoke City. Wanamkosa mchezaji aina ya
(Patrick) Vieira na Gilberto Silva” alisema. kwa upande mwingine Henry anaamini
Arsenal ilifanya kosa kubwa kumuuza Alex Song.
'Song ni kama
nahodha katika boti. Anawalinda walinzi wakati. Unahitaji mmtu mpambanaji
mwenye kuipandisha timu na pia kusaidia kuwapanga wenzie kwa kufanya madhambi
madogomdogo kama alivyokuwa Claude
Makelele'
kabla ya ushindi huo Arsenal ilikuwa imeambulia alama moja pekee kati ya 21
uwanjani hapo.
Hata hivyo
baada ya pambano hilo, Mfaransa huyo alielezea kushangazwa na kiwango cha timu
hiyo pamoja na umiliki wa 32% pekee
'Arsenal mara
nyingi hupenda kukaa na mpira lakini leo ilikuwa tofauti kwani hawakuwa na
mpira muda mwingi wa mchezo huku umiliki wa 32% pekee ukiwahakikishia ushindi.
'Mtizame Cazorla
alivyong’ara leo (jana), watu wamemtaja Alexis Sanchez lakini usimsahau ni Santi
Cazorla’.
0 comments:
Post a Comment