
MWENYEKITI wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba,
Keptein wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JTWZ), Zacharia Hans Poppe ameteuliwa
kuwa mjumbe wa Baraza la 13 la Michezo la Taifa , BMT.
Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari
katika uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika ukumbi wa mikutan, Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Waziri wa
Habari, vijana, utamaduni na michezo, Dr. Fenela Mkangara amemtangaza Dioniz
Malinzi kuwa mwenyekiti, wakati makamu wake atakuwa Zaynabu Matitu Vullu.
Katibu mkuu ni Henry J. Lihaya, wakati wajumbe
waliochaguliwa ni Leonard Thadeo, Alex Mgongolwa, Jamal Rwambo, Adam Mayingu,
Jenifer Mmasi Shang’a, Crecensius Magori, Zainab Mbiro, John Ndumbaro, Zacharia
Hans Poppe na Mohamed Bawaziri.
Mara baada ya kuteuliwa Hans Poppe amemshukuru
Waziri kumpa heshima hiyo na ameaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
0 comments:
Post a Comment