Sunday, January 25, 2015




Gabriel Paulista
Klabu ya Villarreal imetangaza kukubaliana na klabu ya washika mitutu wa London Arsenal kuhusu diri la kumuuza beki wao wa kati Gabriel Paulista huku kiungo mshambuliaji aliyesajiliwa na Arsenal Joel Campbell ambaye amekosa namba katika kikosi cha kwanza akitarajiwa kujiunga na Villarreal kwa mkopo.
mtandao wa Goal mapema wiki hii uliripoti kuwa Arsenal inauwezekano mkubwa kukamilisha diri la mchezaji huyo raia wa brazil, licha ya kuwepo ugumu wa kupata kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza kwa mara ya kwanza.

lakini klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini uhispania imeandika katika mtandao wa twitter kuwa diri hilo sasa linakwenda vizuri na mchezaji huyo kujiunga na Arsenal na kumchukua Campbell kwa mkopo wa mda mrefu.
Joel Campbell

Campbell mwenye umri wa miaka ishirini na mbili alitumaini angepata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal lakini imekuwa ndivyo sivyo na kuambulia dakika 41 tu za michezo ya ligi kuu uingereza msimu huu, huku wachezaji kama Alexis Sanchez, Danny Welbeck na Olivier Giroud wakipambana vikali kugombea namba katika nafasi ya ushambuliaji.

Gabriel atakuwa mchezaji wa pili sasa kusajiliwa na Arsenal mwezi January baada ya kinda mwenye umri wa miaka kumi na saba Krystian Bielik.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video