Thursday, January 29, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salam

Kocha Mkuu wa Mbeya City FC, Juma Mwambusi amesema mabadiliko katika kikosi chake aliyoyafanya kipindi cha mechi yao iliyopita dhidi ya Simba SC, ndiyo 'uchawi' ulioacha kilio Msimbazi.

Simba SC iliyokjwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0, ilipoteza mechi yake ya pili msimu huu ilipopigwa 2-1 dhidi ya kikosi cha City Uwanja wa Taifa jijini hapa jana katika mechi yao ya kiporo cha raundi ya 10 yua Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mechi hiyo ilipaswa kuchezwa Januari 11 Uwanja wa Taifa lakini ikapigwa kalenda na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na ushiriki wa Simba SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 visiwani Zanzibar ilikotwaa ubingwa.

Mara tu baada ya mechi hiyo, Mwambusi alisema mabadiliko aliyoyafanya kwa kuwatoa Themi Felix, Cosmas Lewis na Deus Kaseke kipindi cha pili yalikipa nguvu kikosi chake na kiizidi Simba SC kwa kila kitu.

Alisema kutoka kwa winga mkongwe anayeichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo ya Jiji la Mbeya Ligi Kuu msimu huu, Felix dakika ya 69 ya mchezo kuliamsha mashambulizi mengi langoni mwa wanamsimbazi, hali iliyokifanya kikosi cha Mserbia Goran Kopunovic kipotezane uwanjani.

"Kuna tatizo la marefa, wakati mwingine wanafanya maamuzi kwa kushinikizwa na wachezaji, ninafikiri kipa wa Simba (Manyika Peter) alitakiwa kutolewa kwa kadi nyekundu.

Juma Mwambusi

"Mabadiliko tuliyofanya kipindi cha pili kwa kuwaingiza Hamidu (Mohamed), Idrisa Rashid na (Peter) Mapunda yalikipa nguvu zaidi kikosi chetu ndiyo maana kikawa kinafanya mashambulizi mengi na ya hatari na hatimaye kupata magoli," alisema Mwambusi.

Kocha Bora wa VPL msimu uliopita, Mwambusi alisema anaamini kikosi chake kitaendelea kufanya vizuri kwa vile kimerejesha makali yake ya msimu uliopita baada ya kufanya vibaya katika mechi za mwanzoni mwa msimu kikipoteza mechi nne mfululizo dhidi ya Azam FC, Mtibwa Sugar, Mgambo Shooting na Kagera Sugar.
   
Kipigo cha jana, kiliwaacha wachezaji wa Simba SC wakiangulia vilio mithili ya watoto huku kocha wao akiweka wazi kwamba timu hiyo ya Msimbazi haina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Simba SC itakuwa na kibarua kingine kigumu itakaposhuka tena Uwanja wa Tafa Jumamosi kumenyana dhidi ya JKT Ruvu Stars ya Pwani iliyoko nafasi ya tatu katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi 18 sawa na Yanga SC iliyoko nafasi ya pili kwa faida ya tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.

JKT Ruvu Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, mzawa Felix Minziro iliifunga Simba mabao 3-2 katika mechi yao ya mwisho msimu uliopita Uwanja wa Taifa. 

Kikosi cha Minziro msimu huu kinaoonekana kuwa moto wa kuotea mbali kwani ndiyo timu ya kwanza kuwafunga mabingwa waetezi Azam FC waliotwaa ubingwa wa VPL msimu uliopita bila kupoteza hata mechi moja.

Azam FC ilifungwa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Stars Uwanja wa Azam FC jijini hapa Oktoba 25 mwaka jana ikiwa ni kipigo cha kwanza kwa wanalambalamba baada ya kucheza mechi 38 za Ligi Kuu bila kupoteza hata moja.

Bao la kikosi cha Minziro lilifungwa na mshambuliaji hata kwa sasa VPL, Samwel Kamuntu ambaye amefunga mabao manne katika mechi nne mfululizo zilizopita. Kamuntu ana mabao sita kwa sasa msimu huu akizidiwa bao moja na kinara Didier Kavumbagu wa Azam FC.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video