Beki wa Schalke, Benedikt Howedes (kulia) anawindwa na Arsenal
MAJANGA katika safu ya ulinzi ya Arsenal yameifanya klabu hiyo iweke kipaumbele kusajili beki wa kati katika dirisha dogo la mwezi huu januari.
Siku za nyuma, Arsene Wenge alidhamiria kusajili kiungo wa ulinzi, lakini sasa amebadili akili yake.
Nafasi zote zinahitaji kuongeza wachezaji wakati huu Mikel Arteta na beki wa kati Mathieu Debuchy wakiwa majeruhi.
Wenger mwezi huu anaiwinda saini ya beki wa Schalke, Benedikt Howedes au wa Celtic, Virgil van Dijk.
Howedes, ambaye ana thamani ya paundi milioni 15 ni ngumu kumpata wiki chache zijazo kwasababu mwezi ujao Schalke ina mechi ngumu ya ligi ya mabingwa dhidi ya Real Madrid, na nyota huyo ni nahodha na mchezaji muhimu kikosini.
Kama atataka kuondoka, basi inaweza kuwa majira ya kiangazi mwaka huu.
Hata hivyo, Wenger amekiri kuwa Arsenal bado haijapata beki wa kati wa kumsajili mwezi huu wa Januari.
"Dirisha dogo sio supermarket kwamba unaingia ndani na kununua beki'. Amesema Wenger.
0 comments:
Post a Comment