Mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba akipozi katika picha na tuzo yake
Jose Mourinho amesisitiza kuwa bado kuna mambo mengi yanakuja kutoka kwa Didier Drogba katika klabu ya Chelsea na tayari mshambuliaji huyo amesema anataka kubakia Chelsea baada ya msimu huu kumalizika.
Mourinho alisema hayo wakati Drogba anatunukiwa tuzo ya kuwa na mchango wa muda wote katika soka aliyopewa na chama cha waandishi wa habari za michezo.
Hafla hiyo ilifanyika jana jumapili katika Hotel ya Savoy mjini London.
Mourinho alimsifu Drogba, ambaye alijiunga na Chelsea kwa mara ya kwanza kwa ada ya paundi milioni 24 mwaka 2004 kuwa : "Huyu ni mchezaji mwenye thamani ambayo haijawahi kutokea katika klabu" na amesisitiza nyota huyo mwenye miaka 36 akisema 'Bado hajamaliza"
Drogba, akiwa kazini dhidi ya Bradford jumamosi iliyopita
0 comments:
Post a Comment