Ally Mustafa |
KWA mara ya kwanza msimu huu, mlinda mlango namba
moja wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ ameanzia benchi akimpisha Ally Mustafa ‘Barthezi’
katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shootings jioni ya
leo uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Tangu sare ya 2-2 dhidi ya Azam fc katika mechi ya
ligi kuu iliyopigwa desemba 28 mwaka jana, Dida amekuwa katika wakati mgumu
kwani hata katika michuano ya Mapinduzi ambapo Yanga ilitolewa hatua ya robo
fainali, alipoteza uhakika wa namba.
Katika mechi hiyo ‘Dida’ alifanya makosa na
kufungwa goli la kwanza na Didier Kavumbagu wa Azam fc.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm
amemuanzisha Juma Abdul nafasi ya beki wa kulia, wakati kushoto anacheza Edward
Charles.
Mabeki wa kati wanasimama Rajab Zahiri na Kelvin
Yondani. Kiungo wa ulinzi ni Salum Telela, wakati winga wa kulia ni Simon
Msuva.
Dimba la kati kulia (namba 8) ameanza Haruna
Niyonzima ‘Fabregas’.
Mshambuliaji wa kati ni Kpah Sherman na nyuma yake
atacheza Amisi Tambwe. Winga ya kushoto anaanza Mbrazil Andrey Coutinho.
Wachezaji wa akiba ni: Deo Munish, Oscar Joshua,
Pato Ngonyani, Hassan Dilunga, Danny Mrwanda, Mrisho Ngassa na Hussein Javu.
Wakati huo huo kocha mkuu wa Ruvu Shooting
amemuanzisha golini, Abdallah Rashid, beki wa kulia amesimama Michael Aidan na
beki wa kushoto ni Said Madega.
Mabeki wa kati ni George Michael, Hamis Kasanga.
Kiungo wa ulinzi ni Salvatory Ntebe.
Winga ya kulia amesimama Juma Nade, wakati kiungo
namba nane ni Hamis Maulid.
Mshambuliaji wa kati ni Yahya Tumbo, namba kumi ni
Mwita Kemalonge na winga wa kushoto ni Ayoub Chitala.
Wachezaji wa akiba ni: Bidii Husein, Yusuph Nguya,
Frank Msese, Baraka Mtuwi, Juma Mpakala, Abdurahman Mussa na Lambele Jarome.
0 comments:
Post a Comment