Kipa wa Manchester United, David de Gea anahusishwa kujiunga na Real Madrid
LOUIS van Gaal amekiri kuwa kipa anayewindwa na Real Madrid, David de Gea anaweza kuondoka Manchester United---lakini bosi huyo wa Old Trafford atapambana kumbakisha.
Mapema mwezi huu, Van Gaal alisema kipa huyo mwenye kipaji kikubwa ataongeza mkataba, lakini kuelekea mechi ya leo dhidi ya Leicester City, amekiri kwa mara ya kwanza kuwa anaweza kuondoka.
"Katika mpira, kila kitu kinawezekana", Van Gaal amesema, alipoulizwa kama Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid watamhitaji alijibu: "Tunataka kumbakisha".
De Gea, aliyepigwa picha akicheza dhidi ya Cambridge katika mechi ya FA, amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu
0 comments:
Post a Comment