Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Juventus Turin na timu ya
taifa ya Ufaransa David Trezeguet ametangaza kutundika daruga katika mchezo wa
soka.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliwika sana akiwa na
klabu ya Monaco katika miaka ya 1990, ubora uliopelekea kusajiliwa na miamba ya
soka ya nchini Italia Juventus ambapo aliitumikia klabu hiyo kwa takribani
miaka kumi mpaka 2000.
baada ya kuondoka ligi kuu nchini Italia almaarufu kama Serie A, Trezeguet alitimkia nchini Uhispania na kucheza ligi kuu nchini humo kisha baadae kwenda nchi za Kifalme za Kiarabu kabla ya kuchezea klabu ya River Plate na kisha kujiunga na Newell Old Boys za nchini Argentina.

0 comments:
Post a Comment