Sunday, January 25, 2015





Kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amesema mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya uingereza Daniel Sturridge yupo chini ya uangalizi mkali wa madaktari kuangalia hali yake na uenda akarejea katika mchezo wa marudiano wa kombe la capital one hatua ya nusu fainali dhidi ya watoto wa Jose Mourinho klabu ya Chelsea the blues.
Sturridge amefanikiwa kutikisa vyavu mara ishirini na moja katika mechi ishirini na tisa alizocheza ligi kuu nchini uingereza msimu uliopita, lakini amekuwa nje ya uwanja akiuguza jeraha la nyama za paja tangu mwezi agosti mwaka jana majogoo hao wa arnifield wakiichapa klabu ya Tottenham  magoli matatu kwa bila.

lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amerudi mazoezini na kocha wake Rodgers alisema mshambuliaji wake atakuwa fiti kuchukua nafasi katika benchi la wachezaji wa akiba dhidi ya Chelsea huku akitarajiwa kurudi rasmi January 31 liverpool itakapokuwa inakabiliana na wagonga nyundo wa London west ham united.

"Amefanya mazoezi vizuri na naamini yupo katika kiwango kizuri cha kurejea uwanjani ," Rodgers aliliambia gazeti la Spoti la BT.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video